Connect with us

Soka

Sibomana hatari Aisee

Achana na taarifa za mgomo zinazoendelea Jangwani,Fowadi ya timu hiyo  ni hatari baada ya kushinda mabao 19 ndani ya mechi tatu huku Mnyarwanda Patrick sibomana,Mrisho Ngasaa wakipachika mabao ya kutosha katika mechi hizo tatu za maandalizi ya msimu mpya mjini Morogoro.

Katika mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Tanzanite fc timu hiyo ilishinda magoli kumi huku Ngassa akipachika mabao matatu(hatrick) huku Sibomana,Bigirimana,Tshitshimbi,Balama,Feisal,Rafael na Balinya wakifunga bao mojamoja pia.

Mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Moro Kids ilimalizika kwa Ushindi wa mabao mawili yakifungwa na Balinya kwa mkwaju wa penati pamoja na Paul Godfrey “Boxer” na mechi ya mwisho dhidi ya timu ya ATN Fc timu hiyo imeshinda jumla ya mabao Saba huku Sibomana akifunga magoli matatu(Hatrick) na mengine yakifungwa na Sadney aliyefunga mawili huku Balinya na Lamine Moro wakifunga moja moja.

Kati ya mabao hayo 19 yaliyofungwa mpaka sasa vinara wa magoli ndani ya klabu hiyo ni Patrick Sibomana aliyefunga magoli manne moja dhidi ya Tanzanite na matatu dhidi ya ATN huku Ngassa akimfatia kwa kuwa na magoli matatu aliyofunga dhidi ya Tanzanite Fc.

Katika jumla ya mechi hizo tatu timu hiyo imekuwa na wastani wa magoli 6 kila mechi kitu ambacho kinaashiria timu hiyo itakua na fowadi kali msimu ujao japo sio kipimo cha kujivunia maana imekutana na timu ambazo ni dhaifu ikilinganishwa na zile zinazoshiriki ligi kuu na michuano ya kimataifa.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka