Home Soka Salvatory Akabidhiwa Pamba Jiji

Salvatory Akabidhiwa Pamba Jiji

by Sports Leo
0 comments

Kocha Salvatory Edward sasa rasmi amekabidhiwa kikosi timu ya Pamba Jiji ya Mwanza ambapo kwasasa atasaidiwa na kocha Henry Mkanwa baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kuachana na Kocha Msebia Goran Kopunovic.

Goran Kopunovic na mabosi wa juu wa timu hiyo wapo hatua za mwisho za mazungumzo ili kumalizana rasmi kwa amani japo pia kwasasa hayupo na timu ila yupo kwa ajili ya kufuatilia mambo yake kabla ya kuondoka Mwanza.

Tayari Salvatory ameanza kutekeleza programu za mazoezi za klabu hiyo akishirikiana na msaidizi wake Henry Mgina ili kuweza kuirejeshea makali timu hiyo ambayo haijapata ushindi wowote katika michezo saba ya ligi kuu ya Nbc nchini.

banner

Goran amekuwa kocha wa tano kufutwa kazi kwenye ligi kuu ya NBC akitanguliwa na David Ouma wa Coastal Union,Yousouph Dabo wa Azam Fc, Fikirini Elias wa KenGold na Paul Nkata wa Kagera Sugar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited