Saba Yanga Waisubiri Mtibwa Dar

0

Licha ya kikosi cha Yanga kuwa safarini mkoani Kagera kuwavaa Kagera Sugar imebainika mastaa saba wameachwa jijini Dar es salaam kuwasubiri Mtibwa Sugar watakaovaana nao Septemba 27.

Mastaa hao saba wameachwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha pamoja na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza ambapo mastaa kama Abdulaziz Makame,Paulo Godfrey,Abdala Shaibu Ninja,Juma Mahadhi pamoja na Adam Kihondo wakiachwa kutokana na kukosa namba huku Farouk Shikhalo pamoja na Mapinduzi Balama waliachwa kutokana na kukosa nafasi.

Yanga itacheza na Kagera Sugar kesho saa kumi jioni katika uwanja wa Kaitaba mjini Kagera mchezo unaotazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na ushindani uliopo baina ya pande zote.

Leave A Reply

Your email address will not be published.