R.I.P Maradona

0

Staa wa soka toka enzi na enzi duniani Diego Maradona amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa moyo ambapo japo alikua akisumbuliwa na maradhi ya ubongo kwa muda mrefu.

Ugonjwa wa kufeli kwa moyo ni moja ya maradhi sugu yanayouwa watu wengi duniani ambapo moyo hushindwa kusukuma damu na kupelekea maji kujaa katika mapafu ambapo kitaalamu huitwa’pulmonary edema’

Dakika chache baada ya kifo chake shirikisho la mpira wa miguu nchini Ajentina lilisibitisha kifo hicho kupitia mitandao yake ya kijamii.

Maradona aliyezaliwa mwaka 1960 ni moja ya nguli wa soka walioacha historia duniani hasa wakati wa kombe la dunia la mwaka 1986 akifunga bao lililoitwa mkono wa mungu.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.