Prince Dube Avunjika Mkono

0

Habari mbaya kwa mashabiki wa Azam Fc ni kuumia kwa mshambuliaji raia wa Zimbabwe Prince Dube jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa chamazi.

Dube alitolewa uwanjani dakika ya 18 ya mchezo ambapo baada ya uchunguzi wa kina imegundulika kuwa staa huyo amevunjika mkono na ataenda kutibiwa nchini Afrika ya Kusini.

Dube licha ya kutofunga katika mechi sita hivi sasa,tayari ameshafunga mabao 6 katika ligi kuu Tanzania bara na kuipelekea Azam Fc kuwa na alama 25 katika nafasi ya pili.

Leave A Reply

Your email address will not be published.