Connect with us

Soka

Pitso Aondoka Al-Ahly

Kocha wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri Pitso Mosimane ameamua kuachia ngazi kuifundisha klabu hiyo baada ya kuomba kwa uongozi wa klabu hiyo sababu kuu ikiwa ni kuridhishwa na mafaniko aliyopata klabuni hapo kwa misimu miwili aliyokaa hapo.

Pitso alifanya kikao na mabosi wa juu wa klabu hiyo ambao waliridhia kazi yake na kumtaka aendelee kuifundisha klabu hiyo lakini kocha huyo aliomba kuachia nafasi hiyo kwa kigezo cha kuridhika na mafanikio yake jambo ambalo lilikubaliwa na mabosi hao.

Kocha alikua na wakati mgumu klabuni hapo akikutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wachambuzi na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo ambao walikua wamemuandama wakikosoa mbinu zake za ufundishaji.

Takwimu zake akiwa na timu hiyo ni kama ifuatavyo:

Mechi: 97
Kushinda: 65
Kupoteza: 10
Sare: 22

CAF Champions League 🏆🏆
CAF Super Cup 🏆🏆
Egypt Cup 🏆
Bronze Medal Club World Cup 🥉🥉

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka