Njooni Uwanjani-Jerry Muro

0

Msemaji na Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga Jery Muro amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kushuhudia burudani kutoka kwa mabingwa hao wa kihistoria katika mchezo dhidi ya Gwambina.

Muro ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, yuko likizo na ameamua kuitumia likizo yake kuungana na viongozi kurejesha amsha-amsha ya ushindi klabuni hapo.

Akiwa sambamba na viongozi waandamizi wa Yanga katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Muro amesema amerejea na password ya ushindi Yanga.

“Nawaambia mashabiki kesho njooni kwa wingi uwanjani kuna suprise yenu,” amesema

“Kesho tunafungua ukurasa mpya kwa klabu yetu. Tumezungumza na kocha, wachezaji na tumewaambia kesho afe beki afe kipa, tunataka ushindi”

“Ile kampa kampa tena tunaitaka kesho, tunataka ushindi wa kuanzia goli nane”

“Viongozi wametimiza wajibu wao, wachezaji watimize wajibu wao na sisi mashabiki tutatimiza wajibu wetu”

“Kuanzia leo tunasema kulia basi, hatutakubali kuonewa wala kuhujumiwa na mtu yeyote. Leo tutalinda uwanja, wale waliozoea kutuhujumu waje waone. Hatutajali uwe mwenzetu, au yeyote, tutakushughulikia”

Muro amewataka wadau wote waliokuwa viongozi wa timu hiyo kipindi cha nyuma, wajitokeze kuunganisha nguvu

“Wale wote tuliokuwa sote wakati ule njooni tuunganishe nguvu. Viongozi wamefungua milango, tusibaki kulalamika tu kuwa timu inapotea. Wale mliokuwa mnamwaga upupu njooni mmwage, mliokuwa mkitoa magari, fedha njooni tufanye kazi tuirejeshe heshima ya klabu yetu”

Leave A Reply

Your email address will not be published.