Connect with us

Soka

Mzamiru,Kibu Watozwa Faini

Wachezaji wa klabu ya Simba Sc, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wametozwa faini ya Tsh 1,000,000 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mlango wa Coastal Union, Ley Matampi lililokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.

Taarifa iliyotolewa na bodi inayasimamia ligi kuu nchini imesema kwamba wachezaji hao walifanya kosa hilo katika mchezo baina ya timu hizo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambapo Simba sc ilipata ushidi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Fredy Michael na Willy Onana.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 ya ligi kuu inayohusu udhibiti wa wachezaji ambapo mpaka sasa wachezaji wengi hususani timu za Simba Sc na Yanga sc wamepigwa faini kutokana na makosa hayo ama yanayofanana na hayo.

Mpaka sasa klabu ya Simba sc ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 42 katika michezo 18 ya ligi kuu huku Yanga sc ikiwa kileleni na alama 49 katika michezo 18 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka