Connect with us

Makala

Mwenda Aigomea Singida Black Stars

Beki wa zamani wa klabu ya Simba Sc Israel Mwenda amegoma kujiunga na kambi ya timu ya Singida Black Stars iliyomsajili hivi karibuni kutokana na kutomaliziwa fedha za usajili walizokubaliana.

Awali beki huyo alikubaliana na Singida Big Stars kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 200 ambapo alitanguliziwa kiasi cha shilingi milioni 140 huku akiahidiwa kumaliziwa kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 60 hapo baadaye.

Beki huyo mpaka sasa hajajiunga na timu hiyo akishinikiza kumaliziwa fedha hizo kwanza ndio ajiunge huku mabosi wa klabu hiyo wakigoma kumalizia kwa madai kuwa atamaliziwa atakapojiunga na timu kama mastaa wengine.

Hata hivyo mchezaji huyo amenikuliwa akifanya mahojiano na baadhi ya vituo vya radio ambapo amesema kuwa klabu hiyo imekiuka makubaliano na yuko tayari kuvunja mkataba huo.

Pia taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wamemwandikia barua mchezaji huyo kuripoti kambini ndani ya masaa 24 huku wakituma nakala katika Shirikisho la soka nchini (TFF).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala