Connect with us

Soka

Mwakalebela Akomali Kesi Ya Morrison,Kabwili

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga sc Frederick Mwakalebela ameliibua tena upya suala la kesi ya winga Benard Morrison baada ya kuwa na ukimya wa muda mrefu kwa Shirikisho la soka nchini(Tff) kuamua kuhusu kesi hiyo.

Mwakalebela ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzifanyia kazi kesi zao walizo ziwasilisha ambazo ni ile ya Ramadhani Kabwili, pamoja na mkataba wa Bernard Morrison kwa kuwa wanaelekea katika dirisha dogo la usajili.

Mwakalebela ameongeza kuwa kama suala la Morrison ambalo limefikishwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ya FIFA (CAS) kama lisipofanyiwa kazi mpaka dirisha la usajili likafunguliwa huenda mkataba ukabadilishwa kwa kuwa muda utapatikana dirisha likiwa wazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Soka