Connect with us

Soka

Mudathir,Feisal Wasalimika Kifungo

Wachezaji Feisal Salum wa Azam Fc na Mudathir Yahya Abass wa Yanga sc wameepuka adhabu ya kufungiwa na bodi ya ligi baada ya kufanya kosa la kutosalimiana na wachezaji na waamuzi wakati wa mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo siku ya Jumatatu Oktoba 23 mwaka huu.

Katika mchezo huo baada ya timu zote mbili kuingia uwanjani na kujipanga kwa ajili ya ukaguzi na kusalimiana mastaa hao walibaki nje ya uwanja wakitegeana kuingia kila mmoja mpaka vikosi hivyo vilipomaliza kusalimiana ndipo akaanza Mudathir kuingia uwanjani na Feisal akafuatia.

Kwa mujibu wa kanuni kanuni ya 41:5 (5.4) kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani, kukataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa au kuonesha ishara inayoashiria matusi ambapo adhabu yake inaweza kuwa faini,kufungiwa ama vyote kwa pamoja.

Bodi ya ligi kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma imeamua kuwatoza faini ya shilingi milioni mbili kila mmoja kutokana na kosa hilo huku ikiwaachia huru bila kuwafungia tofauti na matarajio ya wengi.

Kutokana na hilo Mudathir Yahya atakuwepo katika mchezo wa watani wa jadi baina ya klabu yake dhidi ya Simba sc utakaofanyika siku ya jumapili Novemba 5 huku suala la kucheza ama kutocheza likibaki kwa kocha Miguel Gamondi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka