Connect with us

Soka

Msuva Kipaumbele Yanga sc

Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva ameipa kipaumbele klabu ya Yanga sc endapo ataamua kusalia nchini kucheza katika klabu mojawapo ya ligi kuu kutokana na kutokumalizika kwa sakata lake la mgogoro dhidi ya waajiri wake Wydad Casablanca ya nchini Morroco.

Msuva mpaka sasa anasubiri maamuzi ya mahakamya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya michezo (Cas) iamue kesi yake baada ya kuishtaki klabu hiyo kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya kimkataba hasa kutomlipa fedha yake ya usajili.

Kutokana na kesi hiyo ilimbidi Msuva arejee nyumbani kusubiri uamuzi wa mahakama hiyo ambapo klabu kadhaa za ligi kuu nchini zimekua zimfata staa huyo kumuomba achezee moja ya timu kubwa hapa nchini lakini staa huyo anabainisha kuipa Yanga sc kipaumbele zaidi.

“Kama ningekuwa nataka kucheza mpira nyumbani ningekuwa tayari nimeshasaini kwa sababu nimefuatwa zaidi ya mara tano na viongozi wa klabu mbalimbali, ikiwemo Simba, Yanga pamoja na Azam, wameonyesha kunihitaji,”

“Napenda kuwa muwazi kuwa bado ninamalengo ya kuendelea kucheza mpira nje ya nchi ni vile tu hapa kati nimekumbana na changamoto ambazo zimenifanya kurejea nyumbani kwa muda lakini ninaimani kuwa haya ni mapito hivyo yatapita na maisha yataendelea,”Alisema

Msuva aliwahi kupita Yanga sc ambapo alianzia akiwa kinda baada ya kusajiliwa akitokea Moro United ambapo baada ya kukaa Yanga sc takribani misimu mitano ndipo alipoamua kwenda nchini Morroco katika klabu ya Difaa al-Jadid ambayo baadae ilimuuza kwenda Wydad Casablanca.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka