Connect with us

Soka

Mpira Mkubwa sana

Derby ya Kariakoo iliyowakutanisha mahasiu wawili Yanga sc na Simba sc imemalizika kwa sare huku kila upande ukiwa umelizika na matokeo pamoja na viwango vya timu zote mbili kutokana na mbinu zilizotumika uwanjani.

Makocha Cedrick Kaze na Pablo Franco waliingia na mbinu za kushambulia kwa tahadahari wakitumia mifumo ya 4-2-3-1 huku kwa upande wa wenyeji Yanga sc wakianza na Djigui Diarra,Djuma Shabani,Kibwana Shomari,Dickson Job,Bakari Mwamnyeto,Yannick Bangala,Khalid Aucho,Jesus Moloko,Feisal Salum,Fiston Mayele na Saido Ntibanzokiza na wageni Simba sc walianza langoni na Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Joash Onyango na Henock Inonga.

Eneo la kati mwa uwanja walikuwepo Jonas Mkude,Sadio Kanoute,Pape Sakho,Cletous Chama na Chris Mugalu pamoja na Bernad Morrison ambaye hakua na mchezo mzuri huku akinusurika kupata kadi nyekundu kutokana na tukio la awali la kudundisha mpira akipingana na maamuzi ya refa Ramadhani Kayoko.

Yanga sc walijitahidi kushambulia kwa kushtukiza lakini kukosa umakini kwa mawinga Moloko na Saido kuliua mashambulizi mengi huku wakishindwa kumhudumia Fiston Mayele ipasavyo kiasi cha kuwekwa mfukoni na Onyango pamoja na Inonga huku pia kukosa umakini kwa Dennis Nkane kuliwanyima Yanga sc nafasi mbili za wazi.

Simba sc walikwamishwa na Chama ambaye hakua na utimamu wa mechi baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na kukosa mechi za kimataifa huku Pape Sakho akidhibitiwa kwa kutopewa eneo kubwa la kukimbia na mpira hivyo kujikuta muda mwingi akilazimika kupiga pasi za nyuma pekee.

Suluhu hiyo inaendelea kuipa uongozi klabu ya Yanga sc kileleni kwa alama 55 huku Simba sc ikifuata ikiwa na alama 42 ikiwa na mchezp mmoja mkononi huku ikitarajiwa tena timu hizo kukutana katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho endapo Simba sc itaifunga Pamba sc.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka