Morrison Mpaka Kesho

0

Ile kesi iliyoshika nyoyo za wapenzi wa soka nchini hasa wa klabu za Simba sc na Yanga sc kuhusu usajili wa mchezaji Benard Morrison itaendelea tena kesho baada ya leo kushindwa kutolewa maamuzi licha ya pande zote mbili kusikilizwa.

Awali taarifa zilidai kuwa mchezaji huyo ni mali ya Yanga sc baada ya tetesi kudai klabu hiyo imeshinda kesi hiyo lakini mpaka tunaingia mitamboni huku kikao kikiisha bila hukumu hiyo kusomwa rasmi.

Kesi hiyo ya mgogoro wa kimkataba kati ya klabu hiyo na Benard Morrisson imeteka nyoyo za wapenzi wengi wa soka hasa baada ya staa huyo kusaini klabu ya Simba sc ambayo imemtambulisha rasmi kama mchezaji wao.

Leave A Reply

Your email address will not be published.