Connect with us

Soka

Molinga Aponea ChupuChupu

Ni kama zali la mentali baada ya mshambuliaji wa Yanga David Molinga kuponea chupuchupu kutemwa baada ya kurejeshwa kikosini dakika za mwisho wakati wa dirisha la usajili lililofungwa wiki hii.

Iko Hivi,baada ya kuja kwa kocha mpya Luc Aymael ambaye aliangalia video za mechi zilizopita na kuuliza alipo mshambualiaji huyo mwenye mabao 5 katika timu hiyo na kujibiwa ameachwa kutokana na matatizo ya kinidhamu ndipo alipoagiza mchezaji huyo arejeshwe kikosini haraka.

Kwa mujibu wa Aymael,Mchezaji huyo ameona ana msaada katika timu hiyo kufuatia aina ya uchezaji wa staa huyo kuona unaweza kuisaidia timu hiyo hivyo kumrejesha haraka kuungana na timu.

Yanga imewatema wachezaji kadhaa hasa mastaa iliyowasajili msimu uliopita kama Juma Balinya,Sadney Urikhob,Mustapha Selemani,Mybin Kalengo na Issa Bigirimana huku ikiwatoa kwa mkopo Ali Hamad Ali,Rafael Daud na Cleofasi Sospeter.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka