Mashuti Kwanza-Zlatko

0
Kocha mkuu Yanga Zlatko Krmpotic amekuwa akiwahimiza wachezaji wake kupiga mashuti makali wanapokaribia katika lango la wapinzani.
Katika kulithibitisha hilo timu hiyo imeanza majatibio ya kupiga mashuti hayo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandenge ya Zanzibar.
Akizungumzia hilo kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mkoko Tonombe amesema :-
“Unaona kila wakati tunaangalia mbele anataka kuona tunapiga pasi zinazofika ukiweza kupiga ndefu zaidi ni hatua nzuri lakini iwe na uhakika,”alisema Tonombe.
“Anataka pia tupige mashuti pale tunapopata nafasi ya kupiga nafikiri ni kocha mzuri anayelenga kutaka matokeo nafurahi kufanya naye kazi.”
Chanzo:Sportsextra

Leave A Reply

Your email address will not be published.