Connect with us

Soka

Maradona Hoi,Kisa Pombe

Mchezaji mkongwe Diego Maradona ametolewa hospitali siku ya Jumatano, na kuelekea kliniki ya kurekebisha tabia ili kuacha kutegemea pombe. Maradona, aliliongoza taifa lake katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 1986,. Alifanikiwa kufanya upasuaji katika ubongo ili kuondoa kuganda kwa damu, mapema mwezi huu.

Hata hivyo , tatizo la utegemezi wa pombe limemfanya akae hospitalini kwa muda mrefu. “Jambo zuri ni kuwa Diego yuko sawa sasa,” alisema wakili wake, Matias Morla. Wiki iliyopita, Maradona alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires , akiwa anasumbuliwa na anaemia .

Rafiki zake wachache tu ndio waliruhusiwa kumtembelea hospitalini. Wakili wake amesema Diego amepitia kipindi kigumu zaidi katika maisha yake na ilikuwa kama miujiza kukuta damu imeganda katika ubongo wake na angeweza hata kupoteza maisha yake.

Cc:Sammisago

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka