Connect with us

Soka

Manara Kikaangoni TFF

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limempeleka kamati ya maadili Afisa habari wa klabu ya Yanga sc Haji Manara kutokana na kosa la kinidhamu baada ya kurushiana maneno na Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia katika mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho baina ya Yanga sc na Coastal Union jijini Arusha.

Katika mchezo ambao Yanga sc ilishinda kwa penati 4-1 huku tukio hilo likitokea jukwaa kuu ambapo msemaji huyo alizozana na Rais huyo huku klipuza video zikisambaa mtandaoni zikionyesha namna walivyokua wanarushiana maneno huku baadhi ya watu wa Yanga sc akiwemo Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa na Saimon Patrick wakijaribu kumsihi atulie.

Hii sio mara ya kwanza kwa Manara kupelekwa katika kamati ya maadili ya shirikisho hilo la soka ikiwa tayari imeshafanyika mara kadhaa ambapo kuna kipi alifungiwa na kupigwa faini kutokana na makosa hayo ya kinidhamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka