Manara Alipa Faini Tff

0

Mkuu wa idara ya habari na mawasilianao klabu ya Simba sc Haji Manara leo amefika ofisi za makao makuu ya shirikisho la soka nchini (Tff) kulipa faini ya shilingi milioni 5 alizokua amepigwa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji.

Awali kamati yenye kazi ya kutoa maamuzi yenye utatu katika soka nchini iliwapiga faini Manara pamoja na Hassani Bumbuli mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Yanga pamoja na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba sc Zacharia Hanspope.

Manara amelipa faini hiyo katika ofisi za shirikisho la soka zilizopo katika uwanja wa karume kariakoo jijini Dar es salaam na baada ya kufika alishuka katika gari aina ya Harrier yenye rangi nyeusi na aliekea moja kwa moja mapokezi ambapo alienda kulipa faina hiyo.

Leave A Reply

Your email address will not be published.