Man Utd Yapiga 4

0

Klabu ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Istanbul BasakSeher ya nchini Uturuki katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo.

Bruno Fernandes alifunga mara mbili dakika za 7 na 19 na kuweka rekodi ya kuhusika katika mabao 34 katika mechi 35 alizoichezea Man United tangu ajiunge nao akifunga mara 21 na kusaidia upatikanaji wa mabao 13.

Marcus Rashford alifunga kwa penati dakika ya 34 huku Daniel James akifunga pia dakika ya mwishoni na kuifanya United kufikisha alama 9 katika msimamo wa kundi H wakihitaji alama moja kufuzu hatua ya 16 bora.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.