Connect with us

Soka

Man Utd Wapindua Meza

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kumaliza ligi kuu nchini Uingereza kwa kishindo baada ya jana kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City katika uwanja wa King Power.

Mashetani hao wekunu walikua wakihitaji alama moja pekee kumaliza ndani ya nafasi nne za juu ili kupata uhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya walianza kupa bao kupitia kwa Bruno Fernandes dakika ya 71 kwa penati kisha Jesse Lingard kuongeza bao la pili dakika ya 90+6 na kuzima ndoto ya Leicester City waliokua wakihitaji ushindi ili kumaliza katika nafasi nne za juu.

Manchester United wamefanikiwa kufikisha alama 66 na kubaki katika nafasi ya tatu huku Chelsea wakimaliza nafasi ya nne na Leicester City wakimaliza nafasi ya tano huku Liverpool na Man city wakiwa katika nafasi mbili za juu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka