Connect with us

Soka

Man Utd Inajipigia Tu

Manchester United imeibuka kinara  wa kundi L baada ya hapo jana usiku kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Az Alkamaar katika mchezo wa ligi ya ulaya uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

United ililazimika kwenda mapumziko bila bao baada ya wageni kujitahidi kutoa upinzani wa  kutosha lakini kipindi cha pili united ilipata mabao kupitia kwa Ashley Young dakika ya 52 na Mason Greenwood 58′ 64′ huku Juan Mata akipachika bao la nne kwa njia ya penati.

Kwa ushindi huo united imeibuka kinara wa kundi hilo baada ya kuwa na pointi 13 katika michezo sita huku Az Alkmaar akiwa nafasi ya pili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka