Connect with us

Soka

Lwandamina Akomaa na Mwashiuya

Inaelezwa kuwa kocha wa zamani wa Yanga sc Mzambia George Lwandamina ndio kikwazo cha mchezaji Geoffrey Mwashiuya kutosaini timu yeyote hapa nchini akilisikilizia simu ya kocha huyo ambaye anataka akajiunge na Timu anayoifundisha ya Zesco ya Zambia.

Lwandamina anayesifika kwa kutumia wachezaji vijana na kutandaza soka safi aliondoka Yanga na kwenda kujiunga na waajiri wake wa zamani wa Zambia hivyo anamfahamu winga huyo kinagaubaga baada ya kumfundisha jangwani.

Mwashiuya mwenye uwezo wa kucheza winga na mshambuliaji namba mbili(namba 10) anawindwa na baadhi ya timu za ndani kama vile Alliance fc,Jkt Tanzania ambazo hazina budi kumsubiria mpaka mchezaji huyo atakapopata maelekezo kutoka kwa Lwandamina ya ama akajiunge na Zesco au asaini timu nyingine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka