Connect with us

Soka

Lukaku hana furaha Chelsea

Mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Ulaya Chesea Romelu Lukaku amesema kuwa kwasasa hajisikii vizuri kwa kipindi anachopitia ndani ya klabu hiyo kutoaminiwa na kocha wake Thomas Tuchel.

Kauli hiyo aliitoa kupitia mahojiano aliyofanya na kituo cha habari cha skysports Italia ambapo ameeleza mambo mbalimbali anaokabiliana nayo hapo darajani na nini kilitokea wakati anaondoka kwa mabingwa wa soka Italia Inter Milan.

Katika mahojiano hayo Lukaku amesema ”kimwili niko,sina furaha tu na hali inayoendelea lakini ni kawaida,mwalimu ameamua kutumia mfumo tofauti nikiwa kama mchezaji wa kulipwa lazima ni kubaliane nalo,sifurahii hali hiyo lakini sipaswi kukata tamaa hata kidogo”

Mchezaji huyo pia amezungumzia mahusiano yake na klabu aliyotoka ya Inter Milan akisema ”nataka kuwaomba radhi mashabiki wa Inter kwani sikupaswa kuondoka kwa namna ile,nilipaswa kuongea nao kwanza baada ya kila kitu walichonifanyia mimi,familia yangu,mama yangu na mwanangu,sitakuja kusahau,naamini kabisa kutoka ndani ya moyo wangu kuwa nitarejea Inter tena siyo kipindi cha mwisho cha maisha yangu ya soka,bali nikiwa bado na nguvu na uwezo wa kushinda zaidi mataji”.

Kauli hiyo inaonesha kuwa mshambuliaji huyo hafurahishwi na jinsi anavyotumia na kocha wake Tuchel na pengine anawaza kuondoka darajani baada ya kukosa mahusiano mazuri na mkufunzi wake huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka