Connect with us

Soka

Kyombo Njia Nyeupe Simba sc

Mshambuliaji Habibu Kyombo amefanikiwa kuvunja mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Singida Big Stars aliousaini wiki chache zilizopita ambapo amevunja baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili kai yake na timu hiyo.

Awali Singida Big Stars ilimsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo lakini taarifa zinadai baada ya muda mchezaji huyo alisaini Simba sc baada ya kufikia makubaliano hivyo Singida kuamua kuachia picha alizosaini mkataba huo hivyo kuzua sintofahamu kuhusu wapi atacheza msimu ujao baada ya kusaini timu mbili.

Hata hivyo taarifa ya kufurahisha kwa wadau wa soka ni kwamba mchezaji huyo amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Singida Big Stars na sasa atabaki kuwa mchezaji wa Simba sc ambapo ameshasaini mkataba akiwa anasubiri kutambulishwa tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka