Home Soka Kikeke Aula Simba sc

Kikeke Aula Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Simba sc imemteua mtangazaji wa Bbc Salim Kikeke kuwa balozi wa timu hiyo katika jiji la London nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya wadhamini ya klabu hiyo imeonyesha kuwa klabu hiyo imemteua mtangazaji huyo mwenye mapenzi na timu hiyo kuwa balozi katika jiji hilo maarufu duniani.

Kikeke ambaye anaishi nchini humo ataiwakilisha klabu hiyo katika mambo mbalimbali kama mshabiki na mwanachama ambapo moja ya kazi kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inaongeza mashabiki jijini humo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited