Home Soka Jobe,Fredy Hatihati Msimbazi

Jobe,Fredy Hatihati Msimbazi

by Sports Leo
0 comments

Washambuliaji wa klabu ya Simba Sc Pa Omar Jobe na Freddy Koublan huenda huu ndiyo ukawa msimu wao wa mwisho kuonekana katika ligi kuu Tanzania Bara kutokana kutofanikiwa kuonyesha viwango bora katika kikosi hicho mpaka sasa.
Wachezaji hao wakati wanasajiliwa klabuni hapo moja ya kipengele kikubwa katika mikataba yao ni kuonyesha uwezo na kuisaidia timu hasa pindi wanapopata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo na kinyume na hapo klabu inaweza kuamua kuachana nao.
Hata hivyo pia pamoja na mpaka sasa wachezaji hao hawajafanya vizuri huku pia mikataba yao ikiwa inaelekea ukingoni kutokana na kila mmoja kupewa mkataba wa miezi sita kwanza ili kuona uwezo wao.

Kocha Abdelhack Benchika amejitahidi kuwatumia wachezaji hao akiwapa nafasi mara kwa mara japo mara chache sana wameonyesha viwango huku mara nyingi wakikosa mabao ya wazi mara kwa mara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited