Connect with us

Soka

‘Hatumuuzi’ Senzo Asisitiza

Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga sc Senzo Mazingiza amethibitisha klabu hiyo kupokea ofa ya mshambuliaji Fiston Kalala Mayele kuhitajika katika klabu za Kaizer Chiefs inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini na Rs Berkane ya nchini Moroco ambao ni mabingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Senzo ambaye alijiunga na Yanga sc akitokea Simba sc amethibitisha kupokea ofa hiyo za kuhitajika kwa Mayele katika klabu hizo lakini amesisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi kwa maana Yanga sc ipo katika michuano ya klabu bingwa baranin Afrika msimu ujao.

‘ni kweli tumepokea ofa kutoka Kaizer Chief na Rs Berkane kumhitaji Mayele lakini tuna mkataba nae hadi msimu ujao hivyo hatumuuzi’Alisisitiza Senzo ambaye ni Mtendaji mkuu wa kwanza wa Yanga sc baada ya kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu kisasa zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka