Fainali Afcon ni Mane Vs Mahrez

0

Hatimaye baada ya miaka 17 kupita timu ya taifa ya Senegal imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Tunisia bao la kujifunga la Dylan Bronn katika dakika za ziada baada ya dakika 90 mechi kumalizika suluhu.

Timu zote zilipata penati ndani ya dakika 90 za mchezo huku Ferjan Sassi akikosa kwa upande wa Tunisia dakika ya 72 na dakika nane baadae kiungo wa Newcastle ya Uingereza Henry Saivet alikosa penati kwa upande wa Senegali.

Mpaka kipyega cha mwisho cha mwamuzi katika uwanja wa 30 june jijini Cairo kiliwahakikishia vijana wa Aliou Cisse kutinga hatua ya fainali baada ya miaka 17 huku wakijiandaa kuvaana na Algeria.

Mahrez Aivusha Aivusha Algeria

Riyad Mahrez mshambuliaji wa timu ya manchester city naye hakuwa nyuma baada ya kufunga bao dakika za mwisho lililowasaidia Algeria kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria pambano lililopigwa katika uwanja wa kimataifa wa Cairo jumapili usiku.

Krosi ya Mahrez dakika ya 40 ilimfanya beki wa Nigeria Willian Trost-Ekong kujifunga kabla ya Odian Ighalo kuisawazishia Nigeria kwa penati baada ya picha za marudio za VAR(Video assistant Refferee ) kuwazawadia Super Eaggles pigo la penati dakika ya 70 ya mchezo.

Dakika nne za mwishoni mwa mchezo zilitosha kuonyesha utawala wa Riyad Mahrez baada ya kuipatia Algeria goli la ushindi baada ya kupiga faulo iliyojaa moja kwa moja na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Algeria.

Fainali baina ya Senegali na Algeria itapigwa siku ya ijumaa ambapo Algeria itakua fainali yao ya pili katika historia ya timu hiyo huku Senegal ikicheza faainali baada ya miaka 17

Leave A Reply

Your email address will not be published.