Connect with us

Soka

CAF yaitoa Biashara United shirikisho

Shirikosho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limeiondosha rasmi klabu ya soka ya Biashara United ya Mara katika michuano ya kombe la shirikisho baada ya kushindwa kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli.

Biashara ilishindwa kusafiri kucheza mchezo huo uliopaswa kufanyika Novemba 23 nchini Libya kutokana na kile walichodai kukosa vibali vya kutua katika anga za nchi za Sudan na Ethipoia.

Katika mchezo wa awali ulifanyika kwa Mkapa Biashara ilipata ushindi wa magoli 2-0 na kuweka matumaini ya kufuzu mbele.

Taarifa rasmi ya CAF imetolewa na shirikisho la soka nchini(TFF) na kusema kuwa sababu iliyotolewa na Biashara haijitoshelezi kuwafanya kucheza mchezo wa marudiano kwa kusogezwa mbele mchezo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka