Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limeshatangaza mwisho wa kuwasilisha usajili wa wachezaji kwa ajili wa wachezaji kwa timu ambazo zitashiriki mashindano ya CAF (Caf Champion League na CAF Confederation Cup) ni August 15.
Tanzania itawakilishwa na timu 4 ikiwa ni Simba na Yanga zitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya CAF Champion League huku Azam na Biashara zitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya CAF Confederation Cup.
Leo ni tarehe 07/08/2021 zimebaki siku 8 dirisha la usajili la kimataifa kufungwa kwa vilabu vya Tanzania naona timu ya Biashara bado imelala sijajua ni ugeni wa mashindano? au shida nini. Simba walishakamilisha usajili bado kutangaza tu.
Azam walishamaliza bado mmoja kukamilisha tu huku Yanga wao wanamalizia wawili ama watatu wa mwisho ili jeshi lao likamilike ila kwa Biashara ndio shida kuna haja ya TFF kuwakumbusha na kuwasaidia katika hili isije ikafika tarehe 14 ndio waanze kuhaha masuala kusubili deadline sio mazuri.
Pia wanatakiwa kuanza pre-season mapema kwani mashindano ya Afrika yanatakiwa kuanza September 10-12 kwa michezo ya mkondo wa kwanza kwa raundi ya awali (preliminary) na ratiba (draw) nzima ya mashindano ya CAF itatolewa August 15.
CAF imeendelea na utaratibu wa timu kufanya mabadiliko (sub) ya wachezaji watano (5) kwenye mchezo mmoja badala ya watatu (3) pia kwenye bechi wanaruhusiwa kukaa wachezaji tisa (9) badala ya wachezaji saba (7) na kwenye usajili timu inaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi 40 badala ya wachezaji 30.