Buku Tatu Kuiona Simba,Biashara

0

Timu ya Simba sc imetangaza viingilio vya mechi dhidi ya timu ya Biashara United siku ya jumapili ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu tatu.

Katika mchezo huo utakaofanyika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam viingilio vya juu ni shilingi elfu 15000 kwa jukwaa kuu huku jukwaa la V.i.p B kiingilio kikiwa na Shilingi 10000 na lile la V.i.p C kiingilio kikiwa ni Shilingi elfu 5000 na mzunguko ikiwa ni shilingi elfu 3000.

Simba sc imerudi kucheza katika uwanja wa nyumbani baada ya kukamilisha mizunguko miwili kwa kucheza ugenini dhidi ya Ihefu Fc ambapo walipata ushindi wa mabao 2-1 huku wakipata sare katika uwanja wa Jamhuri dhidi ya Mtibwa Sugar.

Leave A Reply

Your email address will not be published.