Connect with us

Soka

Breaking News..Kakolanya Asaini Simba

Aliyekua kipa namba moja wa Yanga Benno Kakolanya amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba Sc akisaini kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Yanga sc kuvunjwa na shirikisho la soka la Tanzania (Tff).

Kakolanya amesaini mkataba huo na kumaliza tetesi za yeye kujiunga na klabu hiyo yenye makao yake makuu Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam huku ikielezwa wakala wake ambaye anafahamika kwa jina la Haroub akicheza nafasi kubwa kufanikisha dili hilo kwa kuwa yeye ni mpenzi wa Simba sc.

Kakolanya alijiunga na Yanga kutokea Prisons ya Mbeya licha ya kutopata nafasi ya kutosha klabuni hapo mbele ya Ally Mustapha na Deo Munishi ambao baadaye waliondoka jangwani na kumuachia ufalme kipa huyo kabla kukorofishana na kocha Mwinyi Zahera aliyegoma kufanya nae kazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka