Connect with us

Soka

Boxer Ajiunga Singida Big Stars

Klabu ya Singida Big Stars imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kulia Paul Godfrey Boxer Kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kuisha.

Beki huyo ambaye alipandishwa katika timu kubwa ya Yanga sc akitokea timu ya vijana na kocha Mwinyi Zahera amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga sc chini ya kocha Nasredine Nabi ambaye humtumia Kibwana Shomari zaidi na Djuma Shabani katika eneo la mlinzi wa kulia huku ikielezwa kuwa klabu ya Yanga sc haikua na mpango wa kumuongezea mkataba mpya.

Singida Big Stars imekua kimbilio la wachezaji wengi wa klabu kubwa nchini baada ya mikataba yao kumalizika wakiwa hawana uhakika wa kuongezewa mikataba mipya na mpaka sasa imehusishwa na mastaa kibao japo tayari imekamilisha usajili wa Aziz Andambwile na Habib Kyombo kutoka Mbeya kwanza Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Soka

 • Halaand Kiboko

  Uongozi wa klabu ya Manchester City upo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wao Erling Haaland...

 • Wa Kawaida Kabisa

  Afisa habari wa klabu ya Yanga sc Ally Kamwe amesema kuwa klabu hiyo haiwahofii...

 • Saido Mambo Fresh Geita Sc

  Kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza tayari amekamilisha taratibu zote kuitumikia klabu ya Geita Golds Sc...

 • Simba sc Yalamba Dili Nono

  Klabu ya Simba sc imefanikiwa kupata udhamini mnono wa kutoka kampuni ya kubashiri ya...