Bado Yupo Sana

0

Rais wa klabu ya Barcelona Jose Bartomeu amesema kuwa anaamini kuwa mshambuliaji wake Lionel Messi kuwa ataongeza mkataba wa mwaka moja licha ya kuhusishwa kutimka klabuni hapo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa anahusishwa kuondoka ndani ya klabu hiyo ya Barcelona hasa baada ya kutokua na msimu mzuri pamoja na kuwa na migongano na viongozi wa klabu hiyo mara kadhaa hasa kuhusu uendeshaji wa timu.

Messi alihusishwa kuondoka baada ya kutokubaliana na mbinu za kocha wa timu hiyo Quique Satien juu ya ufundishaji wa timu hiyo pia aliwahi kukwaruzana na mkurugenzi Erick Abidal.

Leave A Reply

Your email address will not be published.