Connect with us

Soka

Aziz Ki Atwaa Tuzo Oktoba

Bodi ya ligi kuu nchini imemtangaza kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa ligi kuu nchini akiwashinda Moses Phiri wa Simba sc na Maxi Nzengeli wa Yanga sc.

Ki ametwaa tuzo hiyo inayodhaminiwa na Azam Tv ambapo kwa mwezi huo wa oktoba amefanikiwa kufunga jumla ya mabao manne akifunga dhidi ya Geita Gold Fc na mabao matatu akifunga dhidi ya Azam Fc katika ushindi wa mabao 3-2.

Pamoja na Aziz Ki pia kocha wa klabu ya Simba sc Roberto Oliveira ametwaa tuzo ya kocha bora akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga sc na AbdulHamid Moallin wa Kmc ambapo Robertinho alifanikiwa kuiongoza klabu yake kushinda michezo yote ya mwezi huo.

Pia kamati imemchagua Malule Omari kuwa meneja bora wa mwezi baada ya kufanya vizuri katika kuuboresha na kusimamia uwanja wa Highlanders Estates ambao unatumiwa na timu ya Ihefu Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka