Klabu ya Azam Fc imewatema baadhi ya mastaa wa kikosi chake cha kwanza baada ya mikataba yao kuisha hivyo uongozi kuona hakuna haja ya kuendelea kuwa nao katika kikosi kipya kitakachonolewa na Mrundi Ettiene Ndayiragije aliyetokea Kmc.
Miongoni mwa nyota waliotemwa kikosini hapo wapo Obrey chirwa,Ramadhani Singano,Danny Lyanga,Joseph Kimwaga na Hassan Mwasapili pia Twafadzwa Kutinyu aliyetimkia Horoya fc ya Guinnea,Steven Kingu na Mghana Enock Atta Agyei.
Sababu kubwa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ni kuisha kwa mikataba yao japo inafahamika wachezaji wengine wameshindwana kimaslahi baada ya kutaka dau kubwa.
Pia klabu hiyo ya Chamazi jijini Dar es salaam imefanikiwa kuwaongezea mikataba mipya kipa Jackson Haule na Bryson Raphael huku ikimsajili Idd Seleman “Naddo”kutoka mbeya city.
Pia taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kocha mpya Ettiene amehitaji kusajiliwa kwa wachezaji wawili wa kigeni na wawili wazawa hivyo kuwa jumla ya wachezaji wapya anaowahitaji kuwa wanne.