Connect with us

Soka

Azam Fc Yarejea Dar Kuwakabili Yanga sc

Baada ya kugawana alama na Geita Gold Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Nyakumbu mjini Geita klabu ya Azam Fc imewasili salama jijini Dar es salaam ikitokea mwanza tayari kuwakabili Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa mwisho mkoani Geita sare ya 1-1 ilifanya Azam Fc kupoteza alama mbili huku Yanga sc wakiifunga Coastal Union mabao 3-0 mchezo wa mwisho uliofanyika jijini Dar es salaam.

Azam Fc inawalazimu washinde mchezo wa Jumapili ili wafikishe alama 40 na kupunguza pengo la uongozi kwa Yanga sc yenye alama 44 ikiwa na michezo 17 huku ikikumbukwa katika mchezo wa mwisho timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka