Connect with us

Soka

As Vita Kukipiga na Yanga

Klabu ya Yanga sc itawakaribisha timu ya As Vita ya kongo wakati wa kuadhimisha siku ya kilele cha wiki ya mwananchi agosti 4 mwaka huu tukio ambalo litakua la kwanza katika historia ya timu hiyo.

Wiki hiyo ya mwananchi itaanza rasmi tarehe 27 julai ambapo timu hiyo itakua na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa misaada mbalimbali kwa jamii mpaka siku ya tarehe 4 agosti kutakapokuwa na mechi maalumu ya utambulisho wa wachezaji wa klabu hiyo.

GSM WASHINDA TENDA

Pia klabu hiyo katika kuhakikisha inaingiza mapato kutokana na nembo ya klabu hiyo imeamua kuipa tenda kampuni ya Gsm kusimamia usambazaji wa vifaa vya klabu hiyo ikiwemo jezi za klabu hiyo ili kudhibiti wezi na walanguzi waliokua wakijinufaisha bila timu kupata chochote.

Gsm imeshinda tenda hiyo baada ya kushindanishwa na wazabuni wengine na kufanikiwa kukidhi vigezo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka