Connect with us

Soka

Algeria Bingwa Afcon 2019

Timu ya taifa ya Algeria imetwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika baada ya jana kuifunga Senegali 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Cairo.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na msisimuko wa mashabiki iliwachukua Algeria dakika 2 tu kupata goli lililofungwa na Baghdad Bounedjah anayeichezea klabu ya qatar stars baada ya kupiga shuti lililomgonga beki wa Senegali na kujaa nyavuni huku kipa wa Senegali akishangaa.

Senegali walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini kukosekana ubunifu katika eneo la mbele liliongozwa na Niang ilisababisha timu hiyo kukosa nafasi kadhaa za kufunga hali iliyodumu hadi mwisho mwa mchezo licha ya kocha Cisse kufanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza Keprin Diatta na Keita Balde lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.

Licha ya Algeria kutwaa ubingwa pia walifanikiwa kutoa mchezaji bora wa mashindano ambaye ni kiungo Ismael Bennacer aliyesaidia upatikanaji wa mabao matatu katika michuano hiyo huku pia akiwa na mchango mkubwa katika kukaba na kujenga mashambulizi na alikua kikwazo hata kwa simba wa teranga hapo jana.

Kipa wa Algeria Rais M’bohli pia alifanikiwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo wa fainali huku mshambuliaji wa Nigeria Odian Ighalo akiibuka kuwa mfungaji bora baada ya kufunga magoli matano katika michuano hiyo na akiisaidia Nigeria kumaliza nafasi ya tatu.

Kwa ushindi wa jana Algeria imeingia kwenye historia ya timu ilizotwaa ubingwa mara mbili sawa na Ivory coast na Jamhuri ya Kongo huku Moroko,Afrika Kusini na Tunisia zikitwaa mara moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka