Home Riadha Simbu Ashinda Shangai Marathon 2023

Simbu Ashinda Shangai Marathon 2023

by Sports Leo
0 comments

Mwanariadha Mtanzania Alphonce Simbu amefanikiwa  kushika nafasi ya pili katika Shanghai Marathon 2023 na huku Mtanzania mwingine Jackline Sakilu ambaye ameshika  nafasi ya nane katika mashindano hayo maarufu nchini humo.


Pamoja na kupata medali katika mashindano hayo wanariadha  hao wamefanikiwa kufuzu kushiriki Mashindano ya Olympic 2024 na Wataungana na Wanariadha wengine watanzania  Gabriel Gerald Geay na Magdalena Chripine ambao tayari walishafuzu kushiriki Olympic 2024.

Shanghai Marathon ambazo hufanyika nchini china ni moja ya marathon zenye thamani kubwa nchini humo ambazo hufanyika barabarani katika mitaa mbalimbali jijini humo ambapo washiriki zaidi ya elfu moja walishindana katika mbio za kilometa 42.5.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited