Wilder Atemana na Kocha Wake

0

Bondia Deontay Wilder ametemana na kocha wake Mark Breland baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Muingereza Tyson Fury siku ya Jumapili Asubuhi.

Bondia huyo alipigwa kwa TKO raundi ya saba baada ya kocha wake kurusha taulo ulingoni kuashiria kukubali kipigo hicho cha bondia huyo Mmarekani na hicho ndicho kilichosababisha kuachana na kocha huyo.

Pia nyota huyo amezungumzia mavazi aliyovaa kama moja ya sababu ya yeye kupigwa “Hakuniumiza hata kidogo, lakini ukweli rahisi ni kwamba sare zangu ndio zilikuwa nzito sana kwangu,” Wilder alimwambia Yahoo Sports. “Sikuwa na nguvu miguuni tangu mwanzoni mwa pambano. Katika mzunguko wa tatu, miguu yangu ilipigwa kama na butwa hivi. Lakini mimi ni shujaa na watu wanajua kuwa mimi ni shujaa. ”

Leave A Reply

Your email address will not be published.