Connect with us

Masumbwi

Fei Toto Aichezea Jku Zanzibar

Kiungo wa Yanga Feisal Salum Abdallah (Fei toto) asubuhi ya leo Alhamis Disemba 29, 2022 ameichezea Timu yake ya zamani JKU kwenye mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mlandege kwenye Uwanja wa Mao Zedong ambapo JKU walifanikiwa kupata ushindi wa Mabao 4-2 .

Katika mchezo huo Fei alicheza dakika 45 za kipindi cha pili ambapo wakati anaingia Fei JKU walikuwa tayari wapo nyuma kwa Mabao 2-0, lakini baada ya kuingia Fei JKU wakafanikiwa kusawazisha Mabao hayo na kuongeza mengine mawili huku Fei akifunga 1 kati ya Mabao hayo 4 na akiwa na msaada mkubwa wa kupatikana Mabao hayo.

Mwandishi wa Habari hii alifanya jitihada ya kuzungumza na Fei mara baada ya kumalizika mchezo huo lakini Fei aliomba kutozungumza chochote.

“Naomba nisiongee chochote, naomba sana, ikifika siku ya kuongea nitaongea “. Alisema Fei.

Si mara ya kwanza Fei kuonekana kucheza JKU kwani ndio Timu yake ya zamani aliyoondoka mwaka 2018 kabla ya kujiunga na Yanga.

Jumamosi ya Disemba 24, 2022 kupitia mitandao yake ya Kijamii Fei aliwaaga Wanayanga huku timu yake hiyo siku hiyo hiyo ikitoa taarifa yakuwa bado Fei ana mkataba na Yanga mpaka Mei 30, 2024.

Hivi karibuni ziliibuka taarifa ya kuwa Fei huenda akajiunga na Azam FC kutokana na dau nono aliloahidiwa ambapo yeye binafsi aliwahi kusema hachezi mpira kufurahisha Watu bali anacheza Soka kwa kuangalia wapi kuna maslahi.

NB:Taarifa na Mwandishi Abubakar Kisandu,Zanzibar

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi

  • Mwakinyo Huru

    Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) imemfungulia bondia Hassan Mwakinyo kutoka kifungoni baada...

  • Bondia Mtanzania Fadhili Majiha ‘Kiepe Nyani’ ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC Afrika...

  • Ibrahim Class Amtwanga Mchina

    Bondia Mtanzania Ibrahim Class ameshinda pambano la ubingwa wa TPBRC dhidi ya bondia raia...

  • Mwakinyo Aitwa Mahakamani

    Kampuni ya PAF Promotion imemfungulia shauri la madai Bondia Hassan Mwakinyo ambalo linatarajiwa kutajwa...