Yanga,Mtibwa Nani Mbabe Leo?

0

Mtibwa Sugar imekuwa ikipata matokeo mazuri pindi inapokuwa nyumbani dhidi ya Yanga Sc ambapo katika mechi tano za mwisho walizokutana kwenye uwanja huo imeibuka na ushindi mara mbili, sare mara mbili na Yanga imeshinda mechi moja.

Yanga Sc mara ya mwisho kupata ushindi katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ilikuwa Septemba 30, 2015 iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa, lakini baada ya hapo matokeo yaliyofuata ni sare au vipigo.

Maswali mengi yapo leo je nani atanyakuwa pointi tatu muhimu ikiwa mara ya mwisho walikutana na kutoa sare msimu ulioisha wa ligi kuu 2019/2020.

Leave A Reply

Your email address will not be published.