Home Makala Yanga Yamnyemelea Muuaji wa Simba sc

Yanga Yamnyemelea Muuaji wa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga inamfatilia kwa ukaribu nahodha wa timu ya Ud songo ya Msumbiji Luis Miquisson mwenye miaka 24 ambaye huvaa jezi namba 17  pia anaichezea timu ya taifa ya Msumbiji.

Kiungo mshambuliaji huyo ni mchezaji wa Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika ya kusini lakini anaitumikia Ud songo kwa mkopo ambapo timu yake imemtoa kwa mkopo mara kadhaa katika timu za Chipa united, Royal Eagles na sasa Ud songo.

Kiungo huyo ni fundi wa kusukuma mashambulizi kwenda mbele huku akichangiwa na ubunifu katika kupiga pasi za mwisho na kufunga huku pia akiwa na ufundi wa kupiga mipira iliyokufa.

banner

Yanga inafikiria kuongeza mshambuliaji endapo itafanikiwa kufuzu kwenda hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuangukia huko baada ya kutolewa na Zesco united katika kombe la klabu bingwa barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited