Connect with us

Makala

Yanga Yala Miwa Manungu

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mjini Morogoro.

Yanga sc iliyopo juu ya msimamo wa ligi kuu nchini ilihitaji ushindi huo kwa hali na mali ili kutanua pengo la uongozi wa ligi la alama 5 dhidi ya mpinzani wake Simba sc huku Mtibwa ikitaka kujinasua kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ambapo inashika nafasi ya 15 kati ya timu 16.

Yanga sc ikiwatumia Khalid Aucho,Feisal Salum,Salum Abubakari na Saido Ntibanzokiza walitawala eneo la kiungo huku wakikosa nafasi kadhaa za wazi kupitia kwa Dennis Nkane aliyekosa mabao mawili ya wazi akishindwa kumzidi maarifa kipa Jeremia Kisubi.

Iliwalazimu Yanga sc kusuburi mpaka dakika za mwisho kipindi cha kwanza kufunga bao la uongozi kupitia kwa Saido Ntibanzokiza dakika ya 45+3 akipata pasi safi ya Feisal Salum na kupiga shuti kali lililomshinda Kisubi na kujaa wavuni.

Kipindi cha pili juhudi za Saido na Salum Abubakari zilizaa matunda baada ya Fiston Mayele kufunga bao matata kufuatia pasi ya Saido dakika ya 66 na kuwafanya wananchi kushangilia kwa kutetema na mchezaji huyo.

Yanga sc imefikisha alama 39 nane zaidi ya zile 31 za Simba sc huku kila timu ikicheza michezo 15 na kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu nchini huku Yanga sc ikijiandaa kuwavaa Kagera Sugar katika mchezo wa 16 na wa kwanza katika raundi ya pili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala