Connect with us

Makala

Yanga sc,Wasudan Kumalizana Dar

Klabu ya Zalan Fc kutoka Sudan Kusini imeomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kama uwanja wa nyumbani katika mchezo wa hatua ya awali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Yanga sc.

Zalan Fc ambao ni mabingwa wa ligi kuu nchini kwao wamepangwa kucheza na Yanga sc katika mchezo wa kwanza ambao wao ndio wenyeji lakini wakaomba Caf mechi zote zifanyike jijini Dar es salaam kwa maana ya kwao hawana uwanja wenye hadhi ya kuchezewa michuano ya Caf.

Imethibitishwa kwamba ombi hilo limekubaliwa na Caf na sasa michezo yote miwili itapigwa jijini Dar es salaam huku ule wa awali Zalan Fc wakiwa wenyeji na ule wa marudiano Yanga sc watakua wenyeji wa mchezo huo.

Zalan Fc ni timu changa huku ikiwa katika nchi ya Sudan Kusini ambapo hakuna miundombinu mizuri ya soka kiasi cha kushindwa kuwa mwenyeji wa michezo hiyo huku pia suala la bajeti nalo likiwa kikwazo kwao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala