Connect with us

Makala

Yanga sc Yapigwa Faini

Klabu ya Yanga sc imepigwa faini ya jumla ya kiasi cha Shilingi milioni moja na nusu kutokana na makosa ya kinidhamu katika michezo miwili ya ligi kuu ambayo imechezwa mpaka sasa ambapo ilicheza dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha kwa mujibu wa Taarifa ya bodi ya ligi kuu kwa waandishi wa habari.

Katika kosa la kwanza Yanga sc imetozwa kiasi cha Shilingi milioni moja baada ya mashabiki wake kurusha chupa za maji katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta ambapo ni kinyume na kanuni namba 47:1 ya udhibiti wa klabu licha ya klabu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo yakifunga na Fiston Mayele na Bakari Mwamnyeto.

Katika faini ya pili ya shilingi laki tano klabu hiyo imetozwa baada ya kufanya mabadiliko kwa mikupua minne badala ya mitatu kinyume na kanuni 17:32 ya taratibu za mchezo za ligi kuu ambapo kosa hilo lilifanyika katika mchezo dhidi ya Coastal union ambao Yanga sc iliibuka na alama tatu baada ya kushinda 2-0 mabao ya Benard Morrison na Fiston Mayele na hivyo jumla klabu hiyo kutakiwa kulipa jumla ya kiasi cha milioni moja na nusu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala