Connect with us

Makala

Yanga sc Yakomaa na Feisal

Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick amesema msimamo wa klabu kuhusu mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ haujabadilika na kuwa walishafungua milango kwa mchezaji huyo kufuata utaratibu kama anataka kuondoka.
Simon amesema hayo mapema April 12 baada ya kikao cha  kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) iliyokutana kujadili maombi ya Feisal kwa kamati hiyo akiomba mkataba wale na klabu ya Yanga uvunjwe.
Simon aliiwakilisha Yanga kwenye shauri hilo ambalo hata hivyo halikusikilizwa baada ya upande wa Feisal kushindwa kutimiza baadhi ya matakwa ya kisheria hivyo Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena May 04 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kutoka kwenye kikao cha kamati, Simon alisema Yanga haina pingamizi kwa Feisal kuondoka anachopaswa kufanya ni kufuata utaratibu ambao unafahamika duniani kote kuhusu kuvunja mkataba.
“Nafikiri tulishaweka wazi msimamo wetu kupitia taarifa tuliyoitoa huko nyuma. Hatuna pingamizi lolote juu ya Hatma ya Feisal”.
“Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri,” amesema Simon Patrick ambaye pia ni wakili msomi.
Nao wawakilishi wa mchezaji huyo mawakali Fatma Karume na Jasmine Razack alisisitiza kuwa kwa mujibu wa Shirikisho la soka duniani (Fifa) Hakuna sheria kokote dunia inayoamlazimisha mchezaji kucheza bila ridhaa yake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala