Connect with us

Makala

Yanga sc Yaambulia Alama Moja Kwa Jkt

Klabu ya Yanga sc imeshindwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Jkt Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Mbweni jijini Dar es Salaam.

Ikitoka kushinda takribani michezo sita mfululizo ya ligi kuu kwa idadi kubwa ya mabao,pia ilitarajiwa kupata ushindi katika mchezo huo uliokua ukisubiriwa kwa hamu.

Ikianza na kikosi chake cha kila siku kikiwa na mastaa Clement Mzize na Cletous Chama sambamba na Prince Dube ambao waliongoza mashambulizi hayo wakisaidiwa na Pacome Zouzoua sambamba Mudathir Yahaya ambao kipindi cha kwanza walikosa nafasi kadhaa za mabao.

Uimara wa safu ya ulinzi ya Jkt Tanzania ulizidi kupoteza matumaini kwa Yanga sc kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku licha ya mwalimu Hamdi Miloud kufanya mabadiliko ya kuwaingiza Maxi Nzengeli,Stephen Aziz Ki na Kennedy Musonda bado hali ilikua mbaya kwa Yanga sc.

Dakika tisini za mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka mkoani Manyara zilikamilika kwa Yanga sc kupata alama moja ambayo imewafanya kukaa kileleni wakiwa na alama 46 wakicheza michezo 18 ya ligi kuu huku Jkt Tanzania wakiwa nafasi ya tisa ya msimamo wakiwa na alama 20 katika michezo 18 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala